Nzovu "Miaka ishirini inapita na kabila la Wanyamurenge bado halijapata haki yao"

Bw Nzovu akizungumza jukwaani.jpg

Get the SBS Audio app

Other ways to listen

Usiku wa 13 Agosti 2004 takriban watu 166 wali uawa kikatili, na mamia kujeruhiwa ndani ya kambi ya wakimbizi ya Gatumba, Burundi.


Asilimia kubwa ya waathirika na wahanga wa shambulizi hilo, walikuwa wanachama wa Jumuiya ya Wanyamurenge, kabila lawa Tutsi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Jamii hiyo ya Wanyamurenge ambao walikuwa wakimbizi nchini Burundi, wali lengwa kimakusudi na waasi wa Forces Nationales de Libération (FNL), kundi hilo nila wanagambo waki Hutu ambalo limekuwa liki pigana katika vita vya wenyewe kwa wenyewe Burundi.

Wahanga wa mauaji ya Gatumba, wasaidiwa na wafanyakazi kuondoa miili ya jamaa zao walio uawa alfajiri ya 13 Agosti 2004..jpg
Kwa mujibu wa taarifa za wahanga wa mauaji hayo ya kimbari, mamia ya wanamgambo wa FNL wali sikika wakipiga ngoma nakuimba nyimbo za dini zaki Kristo, wakati milio ya risasi ilikuwa ikisikika, watu wakidungwa visu na wengine wakichomwa moto. Msemaji wa FNL alidai uwajibikaji wa shambulio hilo siku iliyo fuata.

Bw Moise Nzovu ndiye Rais wa Shirikisho wa Wanyamurenge wanao ishi Australia. Katika mazungumzo maalum na SBS Swahili, alifunguka kuhusu ukosefu wa haki kwa jamaa na marafiki walio uawa nakujeruhiwa katika shambulizi hilo, licha ya miaka ishirini ya kampeni zaku watafutia haki.

bango la mwaliko wa tukio la maadhimisho ya mauaji ya Wanyamurenge katika kambi ya wakimbizi ya Gatumba, Burundi.jpg
Ukumbi wa Liverpool Catholic Club, utakuwa mwenyeji wa ibada maalum yaku wakumbuka walio uawa naku jeruhiwa katika shambulizi hilo.

Bonyeza hapo juu kwa mahojiano kamili.

Share